Chanzo Kifo cha Michael K Williams Chatajwa

Chanzo Kifo cha Michael K Williams Chatajwa

 

 Usiku wa kuamkia jana ilitokea taarifa mbaya kwa wapenzi wa filamu kutoka nchini Mrekani baada ya taarifa kusambaa zikidai kuwa mwigizaji Michael K Williams amekutwa amefariki katika nyumba yake ya kupumzikia huko Brooklyn.

Mastaa wengi wa Marekani waliipokea taarifa hii kwa mshtuko kwa sababu Michael K Williams alikuwa ni mmoja ya waigizaji pendwa kabisa Hollywood na ilielezwa kuwa alichaguliwa kuja kuigiza maisha ya Rapa DMX.

Hata hivyo mamlaka husika zimesema kuwa moja ya vitu ambavyo vilikutwa nyumbani kwa staa huyo ni dawa za kulevya aina ya Heroin na kuelezwa kuwa alijioverdose.

Sakata la mastaa hao kujioverdose limekuwa likitokea mara kwa mara na kwa mwaka huu limetokea mara ya pili kwani hata kifo cha DMX ilikuwa ameji overdose ingawa DMX alibahatika kukimbizwa hospitalini na ilichukua muda kidogo hadi kupoteza maisha.

Kwa Michael K William ambaye alikuwa na miaka 54  imekuwa tofauti kwani amekutwa amefariki na haijaelezwa kama alikuwa mwenyewe au laah.

Moja ya Tamthilia ambayo alifanya vizuri ni Omar Little ambayo ilianza kuonekana mwaka 2002.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags