Changamoto za wanandoa kufanya kazi sehemu moja

Changamoto za wanandoa kufanya kazi sehemu moja

Na Glorian Sulle

Ndoa ni tukio la kisheria au kijamii na kihisia ambalo linaunganisha watu wawili au zaidi kwa madhumuni ya kuishi maisha ya pamoja. Kwa kawaida ndoa inajumuisha ahadi za kudumu za kujali, kusaidiana na kushirikiana katika maisha ya kila siku, pamoja na kuanzisha familia na kushiriki haki na majukumu ya kisheria kama wenzi wa ndoa.

Maana ya ndoa inaweza kutofautiana kulingana na tamaduni, dini na muktadha wa kisheria wa eneo husika lakini kimsingi inahusu muungano wa kihalali na kijamii wa watu wawili wanaotaka kuishi pamoja na wenzi wao.

Ndoa inachangamoto na faida zake kama ilivyo katika mambo mengine na hii hutokana na mazingira yanayosababisha hali hiyo kwa kuzingatia hayo, mwananchi scoope inaangazia changamoto za wanandoa kufanya kazi katika ofisi moja.

Kukosa mipaka ya kazi na maisha ya ndoa

Ni rahisi kwa majukumu ya ofisi kuathiri maisha ya nyumbani na kinyume chake, kupanga mipaka sahihi kuweza kuwa changamoto, kufanya kazi sehemu moja kama wanandoa inaweza kukuharibia na kuwa changamoto kama hautazingatia mipaka kama mume/mke katika eneo husika.

Sehemu za kazi zina kawaida ya wafanyakazi kuzoeana na kuwa na utani muda mwingi hii huweza kutengeneza hali ya chuki na wivu baina ya wawili hao au baina mfanyakazi na mfanyakazi lakini pia hutengeneza adabu ya woga na hofu hivyo kuathiri utendaji kazi.

Mambo binafsi kuathiri utendaji wa kazi

Mivutano au matatizo binafsi katika ndoa yanaweza kuathiri utendaji kazi ofisini, mfano mume ni bosi na mke ni mfanyakazi katika ofisi hiyo kutokana na ugomvi wa nyumbani mnapofika ofisini kuna uwezekano mkubwa msiende sawa kutokana na kile kilichotokea mkiwa nyumbani hivyo kuleta sintofahamu katika kazi.

Upendeleo katika maamuzi ya kazi

Wanandoa kufanyakazi katika ofisi moja inauwezekano wa kuwa na upendeleo kwa mume/mke wakati wa kupanga majukumu au pale anapokwenda kinyume na utaratibu wa kazi hushindwa kuwajibishana ipasavyo hii hupunguza utendaji kazi katika idara husika hivyo kuathiri taasisi kiujumla.

Majadiliano na mawasiliano magumu

Kutoelewana au kuwa na makwazo madogo katika kazi, hupelekea ndoa kuathirika kwa namna moja ama nyingine hii ni kwa wale wasioweza kutofautisha mambo ya kazi naya familia, hivyo ili kuepuka haya ni vyema mkawa na mipaka ya mambo ya kazi na mambo ya familia au kuwa ofisi mbili tofauti hii itapunguza uwezekano wa kuwa na sintofahau katika ndoa na kazi.

Kukosa faragha

kutokana na kufanya kazi katika eneo moja, wanandoa wanaweza kukosa faragha ya kufanya mazungumzo ya binafsi au kushughulikia mambo binafsi bila kuathiri kazi.

Mfano mnafanya kazi sehemu moja na mke akawa mjamzito kibinadamu maswahibu anayopitia mke katika kipindi hicho mume atamuonea huruma na akatumia muda mwingi kumsaidia baadhi ya shughuli na yeye kushindwa kufanya shughuli zake kwa kiwango kile kinachohitajika hivyo kuathiri utendaji kazi.

Wanaowezakwenda sawa bila kuathiri upande wowote ni wachache sana, ila kwa kushughulikia changamoto hizi kwa maelewano na kuheshimiana, wanandoa wanaweza kufanikiwa kufanya kazi pamoja ndani ya ofisi moja bila kuathiri uhusiano wao.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post