Chadwick kutunukiwa tuzo ya heshima

Chadwick kutunukiwa tuzo ya heshima

Muigizaji kutoka katika filamu iliotamba duniani ya ‘Black Panther’, Chadwick Boseman anatarajia kupokea nyota (tuzo) ya heshima baada ya kifo kwenye Hollywood Walk of Fame mwaka ujao.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Hwdwalkof Fame, wameweka wazi kuwa Chadwick atakuwa mmoja wa watu mashuhuri watakaopokea heshima hiyo mwaka 2024.



Mwigizaji huyo, amewahi shiriki katika filamu kama Da 5 Bloods, 21 Bridges, 42, Ma Rainey's Black Bottom na zingine nyingi.

Wengine watakao ungana na the late Chadwick ni pamoja na Michelle Yeoh, Chris Pine, Kevin Feige, Chris Meledandri, Gal Gadot, Christina Ricci na Maggie Gyllenhaal.

Chadwick alifariki Agosti 28, 2020 huko Los Angeles, California baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags