Celine Dion anatarajia kutumbuiza kwa mara ya mwisho

Celine Dion anatarajia kutumbuiza kwa mara ya mwisho

Mwanamuziki wa Marekani Celine Dion ambaye anasumbuliwa na ugonjwa adimu wa Stiff Person Syndrome (SPS), tangu mwaka 2022 ameripotiwa kupanga kutumbuiza kwa mara ya mwisho katika kipindi maalumu cha Tv.

Celine Dion, licha ya changamoto zake za kiafya, bado ana hamu ya kuimba tena, na kwa sasa anapanga kufanya onesho maalumu la runinga ambalo linaweza kuwa onesho lake la mwisho kuonekana hadharani.

Chanzo kimoja cha karibu cha nyota huyo wa ‘My Heart Will Go On’ kilifichua kupitia gazeti la The Sun na kueleza kuwa “Celine hakati tamaa ya kuimba tena. Amekuwa akifanya kazi na wakufunzi wa sauti, watu wa bendi na wataalamu kwa zaidi ya miezi sita sasa”

Mbali na hayo siku kadhaa zilizopita Celine Dion aliweka wazi ujio wa filamu yake iitwayo ‘I Am: Celine Dion’ inayotarajiwa kuachiwa Juni 25 mwaka huu kupitia Amazon Prime Video, filamu hiyo itaonesha vita yake na ugonjwa huo ambao haujulikani kwa umma.

Celine Dion, mwenye umri wa miaka 55, aligunduliwa na ugonjwa wa Stiff Person Syndrome (SPS) Desemba 2022, na kumfanya aghairishe ziara yake ya Dunia ya Courage.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags