Carl Weathers kutunukiwa nyota ya heshima

Carl Weathers kutunukiwa nyota ya heshima

Marehemu mwigizaji kutoka Marekani Carl Weathers ameripotiwa kutunukiwa nyota ya heshima kutoka ‘Hollywood Walk of Fame’ wiki ijayo, kufuatia na mchango wake katika burudani na michezo.

Kupitia Instagram ya Hollywood imeeleza kuwa nyota huyo wa filamu kama Rocky na Predator ataheshimiwa baada ya kifo chake kwa kupewa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame, Agosti 29 saa 5:30 asubuhi. Hii ni baada ya kufanya makubwa kwenye tasnia ya burudani.

Ikumbukwe kuwa Carl Weathers alizaliwa January 14, 1948 na kufariki Februari 1, 2024 akiwa na umri wa miaka 76 huku sababu ya kifo chake ikitwajwa kuwa ni ugonjwa wa moyo ‘Atherosclerotic’.

CarlWeathers alijulikana kupitia filamu mbalimbali ikiwemo, ‘#Predator’ , ‘#Rocky’, ‘Star Wars’, ‘The Mandalorian’ na nyinginezo.

Mastaa wengine ambao watatunukiwa nyota hiyo ya heshima ni pamoja na nyota wa Black Panther Chadwick Boseman, Rais wa Marvel Studios Kevin Feige, na nyota wa Wonder Woman Gal Gadot, Maggie Gyllenhaal, Chris Meledandri, Chris Pine, Ken Jeong, Mario Lopez, Christina Ricci, Eugene Levy, na Michelle Yeoh.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags