Cardi B atunukiwa tuzo ya muhamasishaji bora mitandaoni

Cardi B atunukiwa tuzo ya muhamasishaji bora mitandaoni

Mwanamuziki kutoka Marekani Card B ametunukiwa tuzo ya muhamasishaji bora mitandaoni katika usiku wa tuzo za ‘Hollywood Unlocked Impact Awards’ zilizotolewa siku ya jana Ijumaa, Juni 21, katika Hoteli ya Beverly Hilton iliyopo nchini humo.

Cardi ametunukiwa tuzo hiyo kuonekana na kuwa mtu mashuhuri ambaye anaongea ukweli pamoja na kuwa na ushawishi katika mitandao ya kijamii.

Cardi sio tu kwamba amekuwa maarufu kupitia nyimbo zake na tuzo za Grammy bali ni mtu wa kutia moyo katika maswala mbalimbali yakiwemo ya kijamii, kisiasa na kimaadili.

Mastaa wengine ambao wameondoka na tuzo hizo katika vipengele mbalimbali na pamoja na Joe Fat, Jasmine Crockett, Jonathan Majors na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags