Cardi B atishia kufuta akaunti zake za mitandao ya kijamii

Cardi B atishia kufuta akaunti zake za mitandao ya kijamii

‘Rapa’ Cardi B kutoka nchini marekani ametishia kufuta urafiki na mashabiki wake na kufuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii baada ya mashabiki hao kudai kuwa ‘rapa’ huyo amerudiana na Offset.

Hii inakuja baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja siku ya jana kwenye matembezi bila ya watoto wao jijini Ney York.

Kufuatiwa na uvumi huo Cardi kupitia mtandao wake wa X alisisitiza kuwa hajarudiana na Offset huku akitishia kuwa-block na kuwa-unfollow mashabiki wake wote wanao shadadia suala hilo.

Cardi B alitangaza rasmi kuachana na Offset mwanzoni wa mwezi Disemba baada ya kudai kuwa anasalitiwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags