Cardi B amkingia kifua Tyla

Cardi B amkingia kifua Tyla

‘Rapa’ Cardi B amemkingia kifua msanii Tyla, aliyekabiliwa na ukosoaji katika mitandao ya kijamii baada ya tukio alilolifanya katika usiku wa Tuzo za Muziki za MTV 2024.

Tyla, aliyeshinda Tuzo ya Muziki ya MTV 2024 katika kipengele cha Afrobeats Bora, wiki iliyoisha wakati wa tuzo hizo alimuomba Lil Nas X amshikie tuzo yake ili aweze kutoa shukrani huku akitania kuwa yeye hayupo kwa ajili ya kushika tuzo hiyo, kufuatia na tamko hilo kitendo hicho kiliwakera mashabiki na kudia kuwa msanii huyo ni mwenye kiburi na majivuno.

Aidha kufuatia na tukio hilo la watu kumshambulia Tyla katika mitandao ya kijamii, Cardi B aliingia moja kwa moja kwenye X Space, akimtetea Tyla kwa kuwataka watu wamuache kwani hawezi kuvumilia kejeli za mashabiki katika mitandao ya kijamii huku akiamini kuwa siku hiyo alilia sana.

“Tyla anatamani asingeweza kushinda hiyo tuzo ya VMA. Kama angejua ingemletea chuki nyingi, ukosoaji mwingi. Nadhani alilia usiku huo.

Mitandao haiwezi kuvumilika. Jinsi mnavyoweza kuchukua picha, kuchukua tukio, na kuligeuza kuwa kitu ambacho siyo, na kumharibu mtu. Mnakosoa sana kiasi kwamba hata hamtambui mnambully msichana huyu, na kama mtafikiria kwa makini, hamna sababu yoyote ya kufanya hivyo, lakini mnafanya hivyo kwa sababu hamumpendi kwa sababu yoyote ile. Mnazidisha sana” alisema Cardi

Aidha aliongezea kwa kuweka wazi kuwa “Nahisi kama mnakuwa wakali sana kwa msichana huyu. Ana miaka 22 tu. Pia, mnajua jinsi ilivyo ngumu kuwa mtu kutoka nchi nyingine anayejaribu kuzoea maisha Marekani?" alimalizia Cardi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags