Cardi B agoma kupiga kura kisa Biden na Trump

Cardi B agoma kupiga kura kisa Biden na Trump

‘Rapa’ kutoka Marekani Cardi B amedai kuwa hatapiga kura katika uchaguzi ujao nchini humo huku akimkataa Rais Joe Biden na mpinzani wake Donald Trump.

Cardi akiwa kwenye mahojiano na ‘Rolling Stone out’ siku ya jana Alhamis, Mei 17, 2024 ameweka wazi sababu ya kutokupiga kura kwa kudai kuwa anaona watu wa Marekani wamesalitiwa kutokana na gharama kubwa za maisha na mishahara midogo.

Hata hivyo mwanadada huyo aliongea machache kuhusu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Donald Trump kuwa asingependa aingea madarakani kutokana na kuiingiza Marekani kwenye shida.

Ikumbukwe kuwa Cardi B katika uchaguzi uliyopita mwaka 2020 akwenda kumpigia kura Rais aliyekuwa madarakani Joe Biden kutokana na sera zake za kurahisisha maisha kwa Wamarekani. Uchaguzi mkuu Marekani wa 2024 unatarajiwa kufanyika Jumanne Novemba 5, 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags