Bushoke: Zuchu namba moja 2023

Bushoke: Zuchu namba moja 2023

Mwanamuziki wa bongo fleva, Ruta Bushoke amemtaja  msanii wa kike, Zuhura Othoman 'Zuchu' kwamba alikuwa namba moja kwa kufanya kazi bora mwaka 2023.

Bushoke ametoa sababu ya mtazamo wake wa Zuchu kufunika mwaka 2023 ni aina ya utunzi wa nyimbo zake zilizokuwa na mabadiliko, yaliyowavuta mashabiki kumpenda zaidi kila alipotoa nyimbo.

"Namanisha kwa upande wa wanawake na wanaume Zuchu kwenye bongo fleva ndiye alifunika na ametoa chachu kwa wengine kufanya kazi kwa ubunifu, ili mwaka huu, muziki uwe na ushindani zaidi sokoni,"amesema na kuongeza.

"Naamini kwenye ukweli ambao utaibua ushindani wa kifikra, kujua walaji wetu wa muziki wanataka kitu gani hasa kwenye ulimwengu wa sasa ambao Dunia ipo kiganjani."

Amesema Zuchu amekuwa na mabadiliko makubwa, anaweza akaimba miziki ya aina nyingi, tofauti na alivyoanza ambapo alionekana akiimba nyimbo kama za aina ya taarabu hivi. Mbali na hilo, Bushoke anatarajia kuachia nyimbo zake mwishoni mwa mwezi Machi, anazoamini zitakwenda kuwapa raha mashabiki wake.

Bushoke anayetamba na wimbo wake wa Chemistry aliyomshirikisha TID, amesema "Kwa ulimwengu wa sasa wenye kiki nyingi, ukitoa kazi yako lazima ujue unatoka na engo gani, ili muziki wako usikike."

Mitandao ya kijamii inasaidia sana, hivyo unawatafuta marafiki  wenye wafuasi wengi ili wakupostie nyimbo zako, pia ubunifu wa kujua ni nyimbo zipi zinazotakiwa."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags