Burna Boy na Ayra kwenye listi ya Obama

Burna Boy na Ayra kwenye listi ya Obama

Kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya watu mashuhuri ifikapo katikati au mwisho wa mwaka huachia ‘listi’ ya ngoma wapendazo kusikiliza, kama ilivyo utaratibu wa ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama tayari ameshusha oradha ya nyimbo azipendazo.

Wasanii waliobahatika kuingia katika ‘listi’ hiyo kutoka Afrika ni pamoja na Burna Boy na wimbo wake mpya wa sittin’ on top of the world’ aliomshirikisha Savage, mwingine akiwa mwanadada Ayra Starr na ngoma yake ya ‘Sability’.

Wakali wengine waliotawala katika orodha hiyo ni Ice Spice, Nicki Minaj, Nas, SZA, Drake, The late 2Pac na wengine kibao.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Obama kwenye post yake hiyo aliacha ujumbe usomekao.

“Like I do every year, here are some songs I’ve been listening to this summer a mix of old and new”.
"Kama ninavyofanya kila mwaka, hapa kuna nyimbo ambazo nimekuwa nikisikiliza msimu huu wa joto , zipo mchanganyiko wa zamani na mpya."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags