Burna Boy, Chloe Penzini

Burna Boy, Chloe Penzini

Wasanii Burna Boy na Chloe Bailey wameingia kwenye tetesi za kimahusiano kufuatia kuonekana kwao karibu hivi karibuni.

Tetesi hizo zilianza baada ya Chloe kutua Lagos, Jumapili Desemba 15,2024 na kupewa mapokezi makubwa. Kisha baadaye akaonekana na Burna kwenye ukumbi wa starehe wakicheza pamoja na mwishowe walitoka mahali hapo wakiwa wameshikana mikono.

Utakumbuka awali, Burna Boy alidaiwa kuwa kwenye mahusiano na rapa wa Uingereza Steflon Don. Hata hivyo kwa upande wa Chloe alikuwa kwenye mahusiano na rapa Quavo.

Lakini pia mapema mwaka huu Chloe alihusishwa kuwa kwenye mahusiano na rapa Gunna baada ya kuonekana kwenye tamasha la Offset wakiwa pamoja, kutokana na hilo Chloe alikanusha uvumi.

Mpaka sasa Chloe na Burna Boy bado hawajathibitisha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags