Burna Boy awatolea povu wanaosambaza picha yake ya zamani

Burna Boy awatolea povu wanaosambaza picha yake ya zamani

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, Burna Boy amewatolea povu baadhi ya watu wanaosambaza na kuinanga picha yake ya zamani akiwa amenyoa ndevu huku akiwataka watu hao kujikita katika mafanikio yake ya muziki na sio kwenye mambo yake binafsi.

Kupitia post yake aliyo-share kwenye mitandao ya kijamii Burna alifunguka kwa kueleza kuwa ni kweli alinyoa ndevu lakini ilikuwa ni mwaka 2021 na siyo hivi karibuni hivyo basi amewataka mashabiki zake kupuuza uvumi huo.

Hata hivyo Burna alimaliza kwa kuzitaka media na blog kujikita katika mafanikio ya wasanii wao na sio kuingilia maisha yao binafsi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags