Bruno wa Singida FG atambulishwa Brazil

Bruno wa Singida FG atambulishwa Brazil

Baada ya kutangaza kuvunja mkataba siku chache zilizopita na ‘timu’ yake ya zamani ya Singida Fountain Gate, kiungo Bruno Gomes ameripotiwa kurejea nchini kwao na kujiunga na ‘timu’ ya Athletic Club inayoshiriki ‘Ligi’ Daraja la Pili nchini Brazil.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amejiunga na ‘timu’ hiyo akiachana na Singida aliyoichezea tangu mwaka 2022. Awali kabla ya kuja Tanzania Bruno aliwahi kuichezea Athletic kuanzia 2018 hadi 2019.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka picha yake ya kutambulishwa ya ‘timu’ mpya, baadhi ya mashabiki wa ‘soka’ nchini wameonekana kumpongeza ikiwa pamoja na ofisa habari wa KMC, Khalid Chuku Chuku aliyemtakia kila la heri nyota huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags