Bongo Movie yapata mtetezi mpya

Bongo Movie yapata mtetezi mpya

Katika miaka ya hivi karibuni, tasnia ya filamu nchini Tanzania, maarufu kama Bongo Movies, imeonekana kukua kwa kiasi fulani. Hata hivyo, licha ya ukuaji huo bado kunaonekana kuna changamoto kubwa katika ushindani wa kimataifa dhidi ya filamu kutoka mataifa mengine.

Hayo yamejionesha kwenye Tuzo za 27 Filamu za Kimataifa Zanzibar 'ZIFF' zilizotolewa Agosti 4 baada ya filamu za Bongo kupigwa za uso na filamu za mataifa mengine. Hii ni kutokana na kwenye kila kipengele ambacho kazi za Bongo ziliingia kuchuana na wasanii wa mataifa mengine kushindwa shindano.

Badala yake tuzo walizoshinda ni zile walizoshindana wenyewe kwa wenyewe kama vile ile ya Mwigizaji Bora wa Kike Tanzania iliyobebwa na Jesca Mtoi kupitia filamu ya
'The Midnight Bride' na Mwigizaji Bora wa Kiume iliyochukuliwa na John Elisha kupitia filamu ya 'Sozi' naweza kusema ni tuzo tatu tu zilizochukuliwa na Bongo movie nikijumlisha na ile ya Filamu Bora Fupi ya Oceanmania/Baharimania iliyoongozwa na Alphonce Haule na Gwamaka Mwabuka

Akizungumza na Mwananchi mwigizaji Hakeem Jumaa, ambaye anacheza kwenye tamthilia ya Dhohar ambayo nayo ilikuwa ikishindania tuzo za ZIFF amesema kinachotakiwa ili kazi za Bongo liweze kuliteka soko la kimataifa ni kuongeza ubora.

"Kitu ambacho kimetukwamisha ni ubora, tuongeze ubora kwenye uandaaji wa kazi zetu, hatukuwa na wakati mzuri kupata ambayo tulikuwa tunatarajia.

"Tuongeze ubora ili tuweze kufanikiwa unaweza kuona umefanya kitu kikubwa kumbe kuna watu wana kizuri zaidi, tujifunze kutoka kwa wenzetu ili wakati mwingine tuweze kufanya vizuri zaidi," amesema

Hata hivyo, akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa Tamasha ZIFF Hatib Madudu amesema kuwa filamu za Bongo hazina shinda yoyote kwani zimekuwa zikishinda kwa miaka kadhaa mfululizo.

"Ukweli ni kwamba filamu za Bongo haz‌ina tatizo lolote huwa zinafanya vizuri sana, kama utakumbuka filamu hizo hazikuwahi kushinda kwa miaka kadhaa zilivyokuwa zinakuja ZIFF, lakini kwa miaka mitatu iliopita ukiacha na mwaka huu, zimekuwa zikishinda kutoka Tanzania, ilishinda Binti (2021), Vuta Nikuvute (2022), na Yonii (2023) miaka yote Watanzania wameshinda kwa kishindo lakini wakati tunashinda na wenzetu wamekuwa wakifanya kazi nzuri ili washinde mwaka huu wenzetu wamefanya kazi vizuri mwakani na sisi tujitahidi ili tuweze kurudi kwenye nafasi yetu,amesema"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post