Bondia Foreman Afariki Dunia

Bondia Foreman Afariki Dunia

Bondia Mstaafu George Foreman amefariki dunia jana Ijumaa, Machi 21, 2025 akiwa na umri wa miaka 76.

Taarifa ya kifo cha Foreman imetolewa na familia yake ambayo hata hivyo haijataja chanzo cha kifo chake.

“Nyoyo zetu zimevunjika. Muhubiri Mchamungu, mume anayejitolea, baba mwenye upendo babu mwenye fahari na mkubwa, ameyaishi maisha yenye imani, uvumilivu na malengo yasiyokoma.

“Muungwana, mwana Olimpiki na mshindi wa ubingwa wa ngumi za juu duniani mara mbili. Aliheshimika sana kwa nguvu ya wema, mtu mwenye nidhamu, imani, na mlinzi wa heshima yake, akipambana bila kuchoka ili kuhifadhi jina lake zuri kwa ajili ya familia yake,” imeeleza taarifa hiyo ya familia ya Foreman.

Foreman alizaliwa Januari 10, 1949 huko Texas Marekani katika familia ya watoto saba iliyolelewa na mama tu aliyetengwa na mumewe huko Kusini mwa Marekani.

Gwiji huyo alikulia katika maisha yasiyo na nidhamu akiacha shule na baadaye kujiingiza katika magenge ya ukabaji watu mitaani ingawa mwishoni aliangukia katika masumbwi.

Ameacha historia ya kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki mwaka 1968 iliyofanyika Mexico akiwa na umri wa miaka 19 na baadaye aligeukia ngumi za kulipwa ambapo alishinda mapambano 37 mfululizo.

Moja ya mapambano yaliyompa chati Foreman ni lile la mwaka 1973 huko Kingston, Jamaica alipomtandika Joe Frazier kwa KO akimuangusha mara sita katika raundi mbili za mwanzo ambapo kabla ya pambano hilo, Frazier alikuwa hajawahi kupigwa.

Pambano maarufu zaidi ni lile la mwaka 1974 maarufu kama 'Rumble in the Jungle' lililofanyika Kinshasa, Zaire ambayo sasa inajulikana kama DR Congo ambapo alipigana na Muhammad Ali ambalo lilikuwa la kwanza kwake kupoteza.

Katika maisha yake ya ngumi za kulipwa, amepigana mapambano 81 ambayo kati ya hayo, 76 ameshinda na amepigwa matano ambapo kati ya aliyoshinda, 68 ni kwa KO.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags