Boateng : Nilishinikizwa kusema Messi ni bora kuliko Ronaldo

Boateng : Nilishinikizwa kusema Messi ni bora kuliko Ronaldo

Mchezaji wa zamani wa ‘soka’ nchini Germany ambaye pia aliwahi kuchezea ‘timu’ ya taifa ya Ghana Kevin-Prince Boaten amefunguka na kudai kuwa aliwahi kushinikizwa kusema Messi ni bora kuliko Ronaldo ili aweze kucheza katika ‘timu’ ya Barcelona.

Kufuatia mahojiano yake na Rio Ferdinand amesema kuwa wakati alipojiunga na ‘klabu’ ya Barcelona aliulizwa kati ya Messi na Ronaldo nani mchezaji bora duniani? huku akilazimishwa kusema kuwa Messi ndiyo bora zaidi la sivyo asingepewa nafasi ya kutechezea ‘timu’ hiyo.

Hii inakuja baada ya kuulizwa swali kuwa ni uongo gani mkubwa aliowahi kuusema katika maisha yake na kueleza kuwa Messi ni bora kuliko Ronaldo licha ya yeye kuamini kuwa CR7 ndiyo bora.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags