Blueface ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela

Blueface ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela

‘Rapa’ Blueface ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mlinzi wa hoteli mwaka 2012 huko North Hollywood.

TMZ iliripoti kuwa meneja wa mwanamuziki huyo, Wack 100, alifanikiwa kuchelewesha adhabu ya Blue kwa miaka kadhaa, lakini baada ya kupatikana na dawa za kulevya hakimu alilazimika kumpa adhabu ya juu zaidi.

Utakumbuka kuwa Blueface alikamatwa na kupelekwa jela ya Van Nuys Januari 12, 2024.

Mbali na mashitaka hayo, Blueface aliwahi kukamatwa kwa wizi Juni 8, 2023, huko Las Vegas, Nevada, Mei 29 alidakwa na polisi tena kwa kuiba simu ya mwanamke kwenye kasino ya Palms, mbali na hayo anakabiliwa na mashitaka ya kujaribu kuua tukio lililotokea Oktoba 2022.

Wakati huo huo, mpenzi wa zamani wa Blue na mama wa mtoto wake, Chrisean Rock, bado yuko jela huko Oklahoma kutokana na mashitaka yanayohusiana na dawa za kulevya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags