Sera ya Jay Z, hatoi pesa kwa ndugu

Sera ya Jay Z, hatoi pesa kwa ndugu

Mwanamuziki bilionea namba moja wa Marekani, Jay Z anaripotiwa kuwa hajawahi kutoa pesa za bure kwa ndugu zake ambao wamekuwa wakimuomba msaada mara kwa mara.

Kwenye moja ya nukuu zake Jigga ameeleza kuwa sera yake ambayo imenyooka na amekuwa akiifuata maisha yake yote ni kutotoa msaada wa kifedha kwa ndugu zake.

“Moja ya sera yangu kubwa ambayo imenyooka haijawahi kupindishwa ni kutotoa pesa bure kwa watu wa familia yangu, kila ninapotembelea familia yangu ndugu wanaleta maombi ya pesa jambo ambalo linanikatisha tamaa sana.

"Na hata nikitaka kupuuza maombi hayo basi watarejea tena baada ya miezi kadhaa na ndio maana nimejifunza kusema hapana na kuweka mipaka katika hili huwa nawaeleza pesa haiji kirahisi inabidi kuifanyia kazi. Muhimu kuwafundisha thamani ya kufanya kazi kwa bidii na heshima katika fedha,”amesema Jay Z.

Mbali na kufichua hilo lakini pia kupitia nyimbo zake kadhaa amewahi kukiri kwamba utajiri unaweza kuleta matatizo na changamoto. Ambapo ameonyesha kupitia muziki wake na mahojiano kwamba kuna migogoro ya kifamilia inayohusiana na utajiri wake.

Katika albamu yake 4:44, Jay-Z alizungumzia kuhusu uhusiano wake na familia yake, hasa mke wake Beyoncé na watoto wao. Lakini pia alitaja changamoto za kifamilia, lakini pia kupitia wimbo wa "Maybach Music 6" na "Success"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags