Ngoma Zilizomkosha Majizzo 2024

Ngoma Zilizomkosha Majizzo 2024

Ikiwa ni desturi ya baadhi ya mastaa na watu mashughuli ku-share orodha ya ngoma walizopenda kusikiliza kwa mwaka mzima, naye mfanyabiashara Majizzo hajakaa kinyonge amedondosha orodha ya ngoma alizopenda kuzisikiliza kwa mwaka 2024.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Majizzo amashare orodha hiyo yenye nyimbo 20 ikiongizwa na wimbo wa Diamond ‘Komasava’ huku akiambatanisha na ujumbe usemao…

“Kwa kuwa mwaka unakaribia kumalizika, nilitaka kushiriki baadhi ya nyimbo ambazo nimekuwa nikisikiliza siku za hivi karibuni na isingekuwa orodha yangu ya nyimbo bila kuhusisha nyimbo za singeli. Natumaini utapata kitu kipya cha kusikiliza,” ameandika Majizzo



Ngoma nyingine ambazo zimeingia katika orodha hiyo ni pamoja na Hakuna Matata, Olodumare, Kautaka, Wivu, Pwita, Ova, Unanichekesha, Dah, Mapozi, Mungu Abless, Tera Ghata na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags