Kesi Ya Lildurk Yasogezwa Mbele Mpaka Oktoba 2025
Kesi inayomkabili rapa wa Marekani Lil Durk iliyopangwa kusikilizwa Januari 7 imehairishwa hadi Oktoba 13, 2025 kufuatia na makubaliano yaliyofanywa kwa pande mbili wanasheria wa Durk na waendesha mashitaka.
Kuhairishwa huko ni kutokana na kufuatilia ushahidi wenye GB 230 za video na picha, kamera za uangalizi pamoja na kurasa 20,000 zenye ripoti ya picha maelezo ya mashahidi na nyaraka za matibabu.
Utakumbuka kuwa kesi hio inahusu madai ya njama ya mauaji ya kukodi ambayo yanamuhusisha LilDurk. Huku mmoja wa washtakiwa wenzake ameripotiwa kukiri kosa.
Kutokana na ugumu na wingi wa ushahidi, muda ulioongezwa unalenga kuhakikisha kuwa pande zote zina nafasi ya kutathmini ushahidi kwa kina na kujiandaa kikamilifu.
Leave a Reply