Aliyefanya Upasuaji Afanane Na Paka, Afariki Dunia

Aliyefanya Upasuaji Afanane Na Paka, Afariki Dunia

Mwanamitandao kutoka Uswisi aitwaye Jocelyn Wildenstein maarufu kama "The Cat Woman" Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Taarifa ya kifo chake imethibitisha na mpenzi wake mbunifu wa mitindo, Lloyd Klein akiweka wazi kuwa mpenzi wake huyo aliaga dunia nyumbani kwake Ufaransa usiku wa Mwaka Mpya huku sababu kifo chake ikiwa ni ugonjwa wa Pulmonary Embolism (kuziba kwa mshipa wa damu kwenye mapafu).

“Tulikuwa na saa nzuri ya furaha usiku huohuo na tulikuwa tukijiandaa kwa ajili ya mwaka mpya, tukachukua usingizi mfupi ili tuonekane wazuri kabla ya kuvalia nguzo za kusheherekea mwaka mwingine, Ni jambo la kusikitisha sana. Ni huzuni kubwa,” alisema Klein

Wildenstein alijipatia umaarufu kwa mara ya kwanza miaka ya 90 baada ya kutalikiana na mumewe mfanyabiashara bilionea wa sanaa, Alec Wildenstein.

Wawili hao walipendana sana ambapo walidumu katika ndoa yao kwa takribani miaka 21, kutokana na Alec na Jocelyn kuwa na mapenzi makubwa na paka ndipo mwanamama huyo aliamua kufanya upasuaji ili afanane na paka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags