Katika maisha yake ya ndondi amefanikiwa kushinda ubingwa wa dunia wa WBC mwaka 1986, kuondoka na mataji ya WBA na IBF, na kuwa bingwa wa bila kupingwa (undisputed heavyweight champion) mwaka 1987-1988.
Mbali na maisha hayo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyatambua kwa miaka yote. Lakini bondia huyo amekutana na changamoto kadhaa katika maisha yake huku akikamatwa na polisi takribani mara 38 wakati alipokuwa mtoto.
Maisha yake ya nyuma
Mike Tyson alizaliwa katika eneo la Brooklyn, New York, na alikulia katika mazingira magumu yenye uhalifu na umaskini. Alikuwa bila baba huku mama yake akifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka 16 baada ya kukosa fedha za matibabu.
Kutokana na ugumu wa maisha alijiingiza katika makundi ya wahalifu akiwa na umri mdogo sana huku ikielezwa kuwa amewahi kukamatwa kwa takribani mara 38 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu mdogo, kama vile wizi, uporaji, na fujo mitaani.
Baada ya kuonekana mtukutu kwa muda mrefu kutokana na kukamatwa na kuachiwa huru polisi walimkamata mara nyingine ndipo wakaamua kumpeleka katika kituo cha kurekebisha tabia cha ‘Tryon School for Boys’, ambako alikutana na kocha wa ndondi Cus D'Amato, ambaye alimsaidia kubadilisha maisha yake na kuingia kwenye ndondi.

Miaka ya 1980, Cus D’Amato alimchukua Tyson kama mwanaye baada ya kugundua kipaji chake akiwa katika kituo cha kurekebisha tabia. Alimfundisha si tu ndondi pia nidhamu na mbinu za kisaikolojia za kushinda wapinzani.
Mbali kukumbana na changamoto hizo alipokuwa mtoto, lakini aliwahi kukamatwa kwa makosa kama unyanyasaji wa kingono mwaka 1992 ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela aliachiliwa baada ya miaka 3.
Kufungiwa kucheza ndondi kwa muda mwaka 1997 baada ya kumng’ata sikio mpinzani wake Evander Holyfield, kukaa saa 24 gerezani (2007), pamoja na kukamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya na kuendesha gari akiwa amelewa mwaka 2006.
Leave a Reply