Mfahamu Mwanaume Aliyenyoosha Mkono Zaidi Ya Miaka 50

Mfahamu Mwanaume Aliyenyoosha Mkono Zaidi Ya Miaka 50

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, kutana na mwanaume kutoka India aitwaye Mahant Amar Bharati Ji ambaye amenyanyua mkono wake wa kulia juu kwa zaidi ya miongo minne (karne 4) miaka 50 kama ishara ya ibada kwa mungu Shiva.

Inasemekana alianza kuunyanyua mkono wake mwaka 1973 kama njia ya kujitolea kikamilifu kwa imani yake ya Kihindu.

Aidha mkono huo unadaiwa kuwa mgumu na umepoteza uwezo wa kushuka kutokana na kutotumiwa kwa muda mrefu huku wengi wakimchukulia kama mtu mwenye Imani madhubuti baadhi yao wakidai kuwa kitendo hicho ni sehemu ya kujitafutia umaarufu.

Kadri muda ulivyopita, misuli yake ilidhoofika, na kumfanya awe hatarini endapo angejaribu kushusha mkono wake kutokana na uwezekano wa uharibifu wa neva.

Hadi mwaka 2023, alikuwa ameendelea na kitendo hicho kwa zaidi ya miaka 50.Hata hivyo, hakuna taarifa za hivi karibuni zinazoonyesha hali yake ya sasa au kama bado yupo hai.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags