Baadhi ya watumiaji wa simu za mkononi wamekuwa wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza kuficha meseji za kawaida kwenye simu zao ili mtu mwingine asizione wala kuzifungua.
Zifuatazo ni njia unazoweza kuzitumia kuficha sms
Kwa watumiaji wa Google Pixel unaweza kutumia programu za App Lock au SMS Lock kutoka Google Play Store ili kuficha au kulinda programu yako ya ujumbe kwa nambari ya siri au fingerprint na hatua zake ni, Nenda kwenye Google Play Store na tafuta AppLock au SMS Lock.
Pakua na sakinisha programu inayokufaa. Fungua programu na weka password au PIN ili kulinda programu zako za ujumbe. Chagua programu za ujumbe unazotaka kulinda (kama vile Messages au WhatsApp).
Baada ya kuweka lock, mtu mwingine atahitaji PIN au fingerprint yako ili kufungua programu hiyo na kuona ujumbe zako.
Aidha kwa watumiaji wa IPhone kuna kipengele cha Hide Alerts ambacho kinaweza kuficha ujumbe na hata zikiingia hazitoonekana kwenye skrini yako.
Hatua za kufanya kwenye iMeseji fungua meseji na tafuta mazungumzo unayotaka kuficha arifa zake. Gusa jina la mtuma jumbe chagua Info, kisha, washa Hide Alerts.
Hii itasaidia ujumbe utaotumiwa kutotokea kwenye skrini yako.

Leave a Reply