Mfahamu Mwanamke Mwenye Akili Zaidi Duniani

Mfahamu Mwanamke Mwenye Akili Zaidi Duniani

Marilyn vos Savant (78) mwandishi na mtaalamu wa kujibu maswali kwa ufasaha kutoka Marekani anatajwa kuwa ndiye mwanamke mwenye akili zaidi duniani kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kufikiri na kutatua matatizo magumu.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo anakiwango cha juu cha akili ‘IQ’ huku akithibitishwa na rekodi ya dunia “Guinness Book of World Records’ ambapo wamemtaja kuwa mwanamke mwenye IQ kubwa kuwahi kurekodiwa.

Akiwa na miaka 10 mwaka 1985, aliweza kusoma na kuelewa masomo ya juu zaidi, jambo ambalo lilifanya familia yake kugundua kwamba alikuwa na IQ ya juu zaidi kuliko kawaida.

Suala hilo lilipelekea wazazi wake kumpeleka kwa mtaalamu wa akili ambaye alithibitisha IQ yake kuwa ni 228, kiwango cha juu kabisa ambacho angetakiwa kuwa nacho mtu mwenye umri wa miaka 23.

Mbali na kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi na kufanya vizuri lakini Marilyn hakufanya kazi nyingi za taaluma aliyosomea ambapo alijikita katika kusaidia na kuwafundisha watu kuelewa baadhi ya vitu huku akijulikana zaidi kwa kuandika maswali na majibu kwenye jarida la Parade.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags