Mfahamu Muosha Magari Mwenye Gharama Zaidi Duniani

Mfahamu Muosha Magari Mwenye Gharama Zaidi Duniani

Kampuni ya ‘Paul Dalton's Miracle Detail’ inatajwa kuwa ndio kampuni yenye gharama zaidi duniani katika uoshaji wa magari. Huku ikitumia dola 15,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 39 milioni katika kuosha gari moja.

Kampuni hiyo ambayo imeanzishwa na Paul Dalton ambaye ndio muoshaji wa magari hayo kutoka Uingereza, anajulikana kwa kutumia mbinu za hali ya juu na bidhaa bora zaidi ili kuhakikisha magari ya kifahari yanapata matunzo bora.

Huduma ambayo inaghariumu kiasi hicho cha fedha

Kwa gharama ya Sh 39 milioni ambayo utaitoa kabla ya gari yako kuoshwa inahusisha usafishaji wa kina wa ndani na nje ya gari. Kung'arisha rangi, na matumizi ya wax maalum inayotengenezwa kwa viwango vya juu vya carnauba (a natural wax).

Vile vile gari lako litaoshwa kwa maji safi na salama ambayo yanadaiwa kuwa zaidi ya maji ya dukani ambayo watu wengi wanakunywa huku uoshaji wa gari ukichukua zaidi ya siku saba hadi 14 kukamilika.

Sheria namba moja ya Dalton ni kutoa huduma kwa wamiliki wenye magari ya kifahari kama Bugatti, Rolls-Royce, Ferrari, Lamborghini, na Aston Martin.

Wateja wake wanadaiwa kuwa ni watu matajiri, wanamuziki, wanasiasa, na watu mashuhuri ambao wanataka magari yao yabaki katika hali bora zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags