Rapa wa Canada, Tory Lanez ametangaza ujio wa album yake ya 'Peterson' inayotarajiwa kutoka March 7, 2025 aliyoiandaa akiwa gerezani.
Licha ya kufungwa kwake, Lanez anaendelea na kazi yake ya muziki na hapo jana amefichua mipango yake ya kutoa albamu mpya. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram rapa huyo amesema anarudi kwa kishindo kwenye muziki mwaka huu 2025 akitangaza kuachia album iliyobeba jina la babu yake 'Peterson'
"This Come Back is Person, Album name Peterson Sequel of Daystar on Friday," ameandika Tory.
Album ya Peterson itakuwa ya kwanza tangu ahukumiwe kifungo hicho Agosti 2024.Licha ya rapa huyo kupokea changamoto kutoka kwa wafungwa wenzake wakimvamia mara kadhaa wakati anarekodi gerezani humo haijamfanya asikamilishe album yake.
Tory lanez ambaye kwa sasa anasota gerezani akitumikia kifungo cha miaka 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga risasi mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni rapa, Megan Thee Stallion mwaka 2020.
Hata hivyo, amekuwa akipambania kupata dhamana bila kupata mafanikio. hivi karibuni ametoa madai yake kuhusu ushahidi uliotumika katika hukumu ya kesi hiyo akisema kuwa alama za vidole na DNA yake havikuwepo kabisa kwenye bunduki iliyohusishwa katika tukio hilo.
"Asilimia tisini ya waliyotumia bunduki hii ni mwanaume na asilimia iliyobaki ni wanawake wawili na mwanaume mmoja. Hakuna hata mmoja wa watu hao wanne ambaye ni DNA yangu. Kwa hivyo, sihusiki kwa 100%, sio sahihi kama walivyosema nilipokuwa kwenye kesi" alisema Tory Lanez kupitia Full Send Podcast.
Wakati huo huo, Megan Thee Stallion hajamaliza vita vyake vya kisheria dhidi ya Lanez na Milagro Gramz, ambapo anamshutumu mwanablogi huyo kwa kueneza habari za uongo kumuhusu akidai ni sehemu ya kupindisha kesi yake dhidi ya Tory.
Timu ya wanasheria ya Megan inasema ushuhuda wake ni muhimu. Wanataka kuchunguza vitendo vya Gramz na madai ya uhusiano wake na baba yake Lanez. Wanadai Gramz alisaidia kueneza video feki na kumnyanyasa Megan kwa niaba ya Lanez.

Leave a Reply