Kila nchi ina misingi na sheria zake. Mara nyingi jina na umaarufu wa mtu si sababu ya kuvunja sheria za nchi fulani. Licha ya kuwa na umaarufu mkubwa lakini wasanii hawa walipigwa marufuku huingia nchi hizi.
1. Beyoncé - Malaysia
Malkia wa muziki Beyoncé, alipigwa marufuku kuingia Malaysia kwa sababu ya mavazi yake yaliyotafsiriwa kuwa siyo ya heshima.
Hiyo ni kutokana na sheria za serikali ya Malaysia zinawataka waigizaji wa kike kuficha miili yao kutoka mabegani hadi magotini na kutoonyesha mipasuo ya mavazi.
Beyoncé anajulikana kwa uigizaji wake, uimbaji wake na hata kujiamini jukwaani jambo linalopelekea kuwavutia watu wengi.
Ikumbukwe Beyoncé amewahi kusitisha matamasha nchini Malaysia mara mbili. Ni 2007 na 2009, kutokana na kanuni za mavazi na maudhui ya matamasha yake.
Makala iliyotolewa mwaka 2016 na Cosmopolitan ilisema kuwa Beyoncé alipigwa marufuku kuingia Malaysia kwa sababu uongozi wa nchi hiyo ulimwona kuwa mchochezi sana. Maonyesho yake yalionekana kudhalilishaji kwa taifa hilo lenye msimamo mkali wa kidini.
2. Jay-Z - China
Jay-Z alipigwa marufuku nchini China mwaka 2006 kwa sababu ya mashairi yake yanayozungumzia bunduki, dawa za kulevya, na madalali wa ngono. Serikali iliona nyimbo zake hazifai kwa vijana.
3. 50 Cent - Canada
Mwaka 2005, rapa 50 Cent alipigwa marufuku kuingia Canada kwa sababu ya tabia yake ya kuimba nyimbo za kuhamasisha magenge "gangsta". Mashairi yake ya vurugu yanadaiwa kuwa tatizo kwa maofisa wa serikali.
4. Akon - Sri Lanka
Akon alipigwa marufuku nchini Sri Lanka baada ya kurekodi video mbele ya sanamu ya Buddha huku wanawake wakiwa wamevaa mavazi ya wazi.
Tukio hilo ambalo lilitokea 2011 lilionekana kama dharau kwa tamaduni za kidini nchini humo lakini hata hivyo mwimbaji huyo aliomba msamaha kwa Wabudha wa Sri Lanka, akisema hakuwahi kuwa na nia ya kuudhi au kunajisi dini ya mtu yeyote na video hiyo, ambayo inaonyesha wanawake wakiogelea mbele ya sanamu ya Buddha.
"Mimi ni mtu wa kiroho, kwa hivyo ninaweza kuelewa kwa nini wameudhika, lakini vurugu kamwe sio jibu na nimekatishwa tamaa kusikia kuhusu kile kilichotokea Sri Lanka,"alisema Akon baada ya kufungiwa kuingia nchini humo.
5. Snoop Dogg - Norway na Uingereza
Norway
Snoop Dogg alipigwa marufuku kuingia Norway baada ya mwaka 2012 kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kjevik akiwa na gramu nane za bangi, pia alikuwa na zaidi ya kiasi cha pesa kisichoruhusiwa kisheria.
Makosa yote mawili yalitosha kwake kupigwa marufuku kuingia Norway kwa miaka miwili na kutozwa faini ya dola 8,600.
Uingereza
Snoop alipigwa marufuku kuingia Uingereza baada ya kukamatwa kwa madai ya machafuko na vurugu tukio hili lilitokea mwaka 2006 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa London Heathrow ambapo wanachama watano wa msafara wake walipigana kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo liliwafanya wafanyikazi kuwaita polisi.
Ugomvi huo uliotokana na wao kukataliwa kuingia kwenye chumba cha mapumziko cha daraja la kwanza cha British Airways. Snoop alipigwa marufuku ya muda usiojulikana kuingia nchini Uingereza.
lakini mwaka wa 2008, jaji wa uhamiaji alitoa uamuzi uliomuunga mkono Snoop lakini hadi 2010 ndipo shtaka la awali kwa msingi wa kuhusishwa liliamuliwa kuwa si la haki kumfungia mtu huyo.
6. Chris Brown - Australia na Uingereza
Chris Brown alinyimwa kuingia Australia na Uingereza kutokana na kesi ya kumpiga Rihanna. Nchi hizi ziliona kuwa matendo yake ya ukatili hayakubaliki.
Mnamo 2015, Chris Brown alipigwa marufuku kuingia Australia kutokana na historia yake ya unyanyasaji wa wanawake. Mwimbaji huyo wa Marekani alipangiwa kuzuru Australia mnamo Desemba 2015.
Hii ilitokana na tukio la 2009, ambapo Brown alipatikana na hatia ya kumpiga na kutishia kumuua mpenzi wake wa wakati huo mwimbaji Rihanna.
Mwaka 2015 Brown alitweet kwamba alitaka kwenda Australia kuhamasisha kuhusu unyanyasaji wa wanawake nyumbani
"Nguvu tuliyonayo kama watumbuizaji inaweza kubadilisha maisha," aliandika Breezy.
Waziri wa Uhamiaji nchini humo Peter Dutton alitangaza kwamba ombi la viza ya Brown imekataliwa Brown alipewa siku 28 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
7. Justin Bieber - China
Justin Bieber alikataliwa kupewa kibali cha kuingia China kwa madai ya tabia mbaya. Serikali ilisema tabia zake hazifai kuigwa na vijana wao.
Justin Bieber alipigwa marufuku kutumbuiza nchini china mnamo 2017 kwa madai ya tabia yake mbaya. Ofisi ya Utamaduni ya Beijing ilitangaza marufuku hiyo ikijibu swali kuhusu kwa nini Bieber hakuratibiwa kutumbuiza nchini china.
Kwa nini alipigwa marufuku?
Masuala ya kisheria. Bieber amekuwa na mijadala mingi na sheria ikijumuisha kukamatwa mnamo 2014 kwa tukio ambalo alishtakiwa kwa kulaghai nyumba ya jirani mnamo 2014.
lakini pia Walidai kuwa Bieber amehusika katika mizozo ya mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na picha aliyoichapisha akitembelea Madhabahu ya Yasukuni huko Tokyo mwaka 2014.
8. Selena Gomez - Russia na China
Selena Gomez, aliwekewa vikwazo nchini Russia na China kwa sababu ya msimamo wake wa wazi kuhusu haki za LGBTQ+. Ujasiri wake wa kuhubiri usawa haukupokelewa vizuri na mataifa haya.
Aidha mnamo 2014, Gomez alichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na Dalai Lama. Picha hiyo ilipigwa wakati wa mradi wa kuwawezesha vijana huko Vancouver.
Dalai Lama aliondoka nchini China na kukimbilia India kuanzisha serikali ya Tibet, Serikali ya China ina msimamo mkali dhidi ya Dalai Lama.
Baada ya Gomez kupiga picha na Dalai Lama alitangaza kufanya show Guangzhou na Shanghai nchini china kama sehemu ya ziara yake ya kimuziki lakini matamasha hayo yaliondolewa kwenye tovuti yake baada ya serikali ya China kumtaka asitishe mara moja.
9. Tyler, The Creator - Uingereza, Australia na New Zealand
Tyler alizuiliwa kwa muda katika nchi hizi tatu kwa sababu ya mashairi yake yanayodaiwa kuhamasisha vurugu dhidi ya wanawake na makundi mengine.
10. Miley Cyrus - China na Dominican Republic
Miley Cyrus alipigwa marufuku nchini China baada ya kudhalilisha watu wa Asia kwa kuvuta macho yake katika picha. Dominican Republic ilimkataa pia kwa sababu ya maonyesho yake yaliyotajwa kuwa machafu.
Leave a Reply