Baada ya miaka 13 ya ndoa 2Face na mkewe watengana

Baada ya miaka 13 ya ndoa 2Face na mkewe watengana

Mwanamuziki wa Nigeria, Innocent Idibia '2Face' ametangaza kutengana na aliyekuwa mkewe Annie Idibia baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 13.

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inamuonesha 2Baba akithibitisha utengano wao.

Kabla ya video hiyo chapisho la kwanza la msanii huyo kwenye mtandao wa Instagram lilisomeka, “Hallo kwa watu wangu wazuri kweli, jambo hili ninalopaswa kusema ni fupi lakini pia refu. Mimi na Annie Macaulay tumetengana kwa muda sasa, na kwa sasa tumewasilisha kesi ya talaka.

Ningetoa taarifa kwa vyombo vya habari hivi karibuni ili kusema hadithi yangu. Sio kwa sababu ni haki ya mtu yeyote kujua kuhusu maisha yangu ya kibinafsi lakini kwa sababu ninawapenda watu wangu na ninahitaji wajue kutokuwa na hatia au kosa langu. Endelea kubarikiwa watu wangu. Nawapenda nyote,” liliandikwa kupitia ukurasa wa 2face

Hata hivyo muda mfupi baadaye, iliwekwa taarifa nyingine kwenye akaunti hiyo ikidai kuwa ukurasa huo ulikuwa umedukuliwa kwahiyo ujumbe huo upuuzwe.

Ilisomeka, “Akaunti yangu ya Instagram imedukuliwa, juhudi zinafanywa kurudisha.Nawapenda!"

Katika hali ya kushangaza, 2face baadaye alitoa video kufafanua hali hiyo na kuweka wazi kuwa akaunti yake haikudukuliwa kama taarifa ya awali ilivyosema, na alidokeza kuwa chapisho la awali kuhusu kutengana na aliyekuwa mkewe lilikuwa la kweli na sasa wapo kwenye utaratibu wa kupeana talaka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags