Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Snoop Dogg amefunguka siri ya kudumu kwenye ndoa yake na mkewe Shante Broadus kwa miaka 27.
Akizungumza na tovuti ya People kwenye moja ya mahojiano yake amesema mke wake huwa anamuelewa sana, anajua namna ya kushughulika na madhaifu yake.
“Yeye ni mzuri katika kuyakabili madhaifu na mabaya yangu, ananielewa sana. Yeye ni mama mzuri, bibi wa ajabu, mke bora, na rafiki mzuri. Anajua jinsi ya kugusa kila kitu cha ndani yangu ili niwe mtulivu na ninapenda hivyo.
"Jinsi gani nimesalia katika ndoa kwa muda mrefu? Nimepata mke mwenye nguvu, mgongo thabiti na moyo mzuri yeye ni mpenzi na anajali, na sisi tulikusudiwa kuwa pamoja. Tuliposema tutaoana, tuliowa mpaka kifo kitutenganishe. Hiyo siyo ndiyo inasema? Sio mpaka mashindano yatutenganishe au mapigano au fedha, bali mpaka kifo kitutenganishe,”amesema Snoop
Alisema mke wake hajawahi kufanyakazi hata siku moja katika maisha yake, na hicho ndicho kitu kingine kinachopelekea amjali.
"Familia ni kila kitu. Kinachoniletea furaha zaidi maishani mwangu hivi sasa ni kuona mke wangu akiwa na furaha, na kila mtu katika familia yangu akiwa na afya nzuri, na kuwa na umoja, ambayo ni upendo,”amemalizia Snoop
Hata hivyo safari ya kuelekea miaka 28 ya ndoa yao ambayo wanatarajia kuitimiza Juni haikuwa rahisi kwani baada ya kuoana mwaka 1997 wawili hao ambao wamejaaliwa kupata watoto watatu na wajukuu. Waliwahi kutengana mwaka 2004 na baada ya miaka minne walirudiana tena.
Leave a Reply