Mashabiki Waendelea Kumnanga Bieber

Mashabiki Waendelea Kumnanga Bieber

Mwanamuziki Justin Bieber ameendelea kupokea maoni tofauti tofauti kutoka kwa mashabiki huku wakimnanga kufuatia na matendo yake ambayo amekuwa akiyafanya kwa siku za hivi karibuni.

Mapema Jana Alhamis Februari 27, 2025 Bieber alishare video kupitia ukurasa wake wa Instagram huku ikimuonesha akiwa anavuta bangi licha ya msemaji wake kukanusha msanii huyo kutumia mawada pamoja na bangi, tukio hilo lilipokea maoni kutoka kwa mashabiki huku wengi wao wakidai kuwa mwanamuziki huyo anahitaji msaada wa kitabibu kwani huwenda anamatatizo anayapitia.

Utakumbuka wiki iliyokwisha msemaji wa Bieber aliiambia TMZ kuwa msanii huyo hatumii dawa za kulevya wala bangi “Hili linaonyesha kuwa licha ya ukweli ulio dhahiri, watu wanaendelea kushikilia simulizi hasi, zenye kupotosha na madhara. Justin Bieber hatumii dawa za kulevya wala kitu chochote kile,” alisema msemaji huyo

Mapema mwezi huu msanii huyo alizua mijadara katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kama mzee wa miaka 40 licha ya kuwa na miaka 30 kwa sasa.

Mwonekano huo umewafanya mashabiki wake kujawa na maswali huku wengi wakionesha kumuonea huruma. Ikumbukwe 2023 msanii huyo alitangaza kusumbuliwa na ugonjwa wa ‘Ramsey Hunt Syndrone’ ambao unapelekea mwonekano wake haswa uso kuoneakana umezeeka kutokana na maumivu na miwasho anayoipata usoni.

Mbali na hayo msanii huyo amewahi kufanya vizuri na ngoma zake kama vile Baby, Sorry, Yummy, Never Say Never, Lonely, One Time na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags