Marvel Studios Kuja Na Filamu Hizi 2025

Marvel Studios Kuja Na Filamu Hizi 2025

Kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa filamu kutoka Marekani, Marvel Studios imeshusha orodha ya filamu ambazo zitaachiwa mwaka 2025.

Kupitia tovuti ya Marvel wametangaza kuja na filamu kama animation ya ‘Spider Man: Your Friendly Neighborhood’ itakayotoka Januari 29, ‘Captain America: Brave new world’ Februari 14, ‘Daredevil: Born Again’ Machi 4, ‘Thunderbolts+’ Mei 2, ‘Ironheart’ Juni 25, ‘Wonder Man’ Decemba na nyinginezo.

Mbali na hizo lakini pia wameweka wazi kuja na muendelezo wa baadhi ya series walizowahi kuziachia ikiwemo Wandavison, Agatha all Along, She-Hulk: Attorney at law, Ms.Marvel, Moon Knight, Let us Know in the comment na nyinginezo nyingi.

Kampuni ya Marvel Studios imekuwa na ushawishi mkubwa duniani kote kufuatia na ubora wa filamu zao walizowahi kutamba nazo ikiwemo Venom, Spider-Man: Homecoming, Punisher: War Zone nk.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags