MAMA MOBETTO AFUNGUKA HAYA BAADA YA NDOA KUPITA

MAMA MOBETTO AFUNGUKA HAYA BAADA YA NDOA KUPITA

Mama mzazi wa mfanyabiashara na mwanamitindo Hamisa Mobetto, Shufaa ameonesha furaha kufuatia na ndoa ya mwanaye huku akiweka wazi tuu anamshukuru Mungu kwa kumletea mkwe sahihi.

“Tangu hili suala linaanza nilikiwa naona kama njozi jinsi gani kwamba vitu vingi tumepitia lakini mimi kitu changu kikubwa huwaga ni kimoja tuu, Allhamdullillah Mwenyezi Mungu amemfikisha leo mwanangu ameshakuwa Mrs Aziz K.


Nampenda sana mkwe wangu hicho ndio kitu ambacho kila mtu nilitamani ajue jinsi gani ninavyo mpenda na nilikiwa namuomba Mwenyezi Mungu kila siku alete mkwe ambaye tutabond yaani yeye na sisi tuelewane, tupendane kwahiyo huu ni wakati sahihi Mwenyezi Mungu kaniletea mkwe sahihi ananipend mimi anamoend Hamisa na watoto wake wote,”amesema Mama Mobetto akifanyiwa mahojiano ya Zamaradi Tv baada ya ndoa kupita


Mbali na hilo ameweka wazi kuwa mwanaye huyo hakulipiwa mahari ya ng’ombe 30 kama mitandao inavyosema bali ametolewa pesa na ng’ombe 150.


“Nadhani ilikiwa live lika mtu ameona ng’ombe jamani wale wamesimama Ng’ombe wameenda kwa mama yangu Mapinga kule tulishatengeneza zizi kwahiyo sijawahesabu nilikiwa bado nina furaha walikuwa ni ng’ombe kama 150 ndio tulio kubaliana. Kwetu ni sheria mimi natoka familia ya chifu kwahiyo sheria yetu unaolewa na ng’ombe,” amesema Mama Mobetto.

Ndoa hiyo imefungwa majira ya saa 8 mchana katika msikiti wa Masjid Nnuur uliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags