Fahamu Haya Kabla Hujaingia Chuo Kikuu

Fahamu Haya Kabla Hujaingia Chuo Kikuu

Na Michael ANDERSON

Wasomi mambo vipi pande za vyuoni? tunakaribia kuanza paper la UE nafahamu tunazima moto kwa energy ya kutosha kuhakikisha SUP haitupati.

Wiki hii nakuletea haya mazuri ya kuyafahamu kabla ya kuingia chuoni lakini yanaweza kuwa msaada hata sasa upo chuoni.

 

FANYA TENDA BADILIKA

1.Hakuna Atakayekukumbusha Kusoma Chuoni

Chuoni tumeshakua watu wazima lecturer hawezi kukupangia muda wa kusoma wala kuingia darasani hivyo lazima uzingatie wewe mwenyewe binafsi kufanya juhudi.

 2.Jifunze Ujuzi Wowote

Tafuta watu wenye ujuzi tenga muda ujifunze baadhi ya juzi ambazo zitakusaidia baada ya chuo na pia hata muda ukiwa chuo itakusaidia kupata mia mbili mia tatu mfano kuendesha boda, ususi, kutengeneza cake kutengeneza juice na mambo mengine

3.Kuwa Na Side Hustle

Ukiwa chuoni hakikisha unakua na side hustle kama biashara ama kitu chochote kitakachokua kinakuingizia pesa huku ukiwa unasoma itakuongezea marafiki connection pamoja na uzoefu baada ya kumaliza chuo unakua na pakuanzia kama sehemu ya maisha

4.Usijaribu Ku-Impress Classmate Wako No Body Cares

Usijaribu kufanya mambo kwa mihemko kuwavutia washikaji ama kushindana na wana chuoni kila mtu ana kwao kila mtu ana maisha yake usifanye vitu uwavutie wengine angalia maisha yako kila siku no body cares shauri lako!

5.Maisha Tunayotoka Ni Tofauti Chunga Sana

Chuoni hatufanani maisha so chunga sana marafiki na watu wako wa karibu kufata mienendo yao usiige maisha ya mtu chuoni maisha ya chuo ni ya muda mfupi sana so hakikisha hawakuchanganyi hata kidogo hao marafiki zako

6.Wazazi Wanajinyima Sana Kwa Ajili Yako

Uwapo chuoni kumbuka wazazi wako wana matumaini makubwa sana na wewe wanafanya namna zote ili uendelee kusoma na kufikia malengo yako usiwaangushe usiwa-disappoint

  1. Sehemu Za Michanganyiko Zina Kasi Ya Maambukizi Cheza Salama

Sehemu  kama za vyuo ni sehemu zenye vijana wengi sana hivyo ni muhimu sana kuwa makini na sehemu hizi kwani maambukizi ya magonjwa ya ngono huwa rahisi sana cheza salama baki na mtu mmoja kwenye mahusiano kuwa na mahusiano yenye thamani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags