Zingatia haya unapotaka kuvaa nguo oversize, oversize

Zingatia haya unapotaka kuvaa nguo oversize, oversize

Kuvaa nguo za oversize (Kubwa) kunaweza kuwa mtindo wa kipekee na wa kuvutia, lakini kuna mambo kadhaa ya kuzingatia ili kuhakikisha unazivaa kwa njia bora na ufanisi. Zingatia vitu hivi

  1. Chagua Nguo Bora

Ingawa nguo za oversize zinapendeza, ni muhimu kuchagua zile zinazokufaa na ambazo zitakupa muonekano mzuri wa umbo lako. Vitu kama suruali au mashati makubwa lazima yawe  mazuri katika muundo wake.

Changanya nguo kubwa na zile zinazokutosha. Kwa mfano, unaweza kuvaa koti kubwa na suruali za slim au fulana ya oversize na suruali zilizobana ili kupata uwiano mzuri.

  1. Rangi na Muundo wa Nguo

Wakati mwingine nguo za oversize zinahitaji kuwa na rangi ya kawaida au zilizochanganyika vizuri. Kama unapenda kuonekana upo kisasa zaidi.

Nguo zenye michoro mingi zinaweza kuficha muonekano, hivyo ni bora kuchagua zenye rangi moja au michoro ya wastani.

  1. Vitu vya Ziada

Kwa nguo za oversize, nyongeza kama viatu vya staha, mikoba midogo, au pete kubwa zinaweza kusaidia kuongeza mvuto. Hakikisha unachagua vitu vinavyovutia 

Kwa baadhi ya mavazi ya oversize, kama suruali au mashati, kuna haja ya kuongeza vitu kama mikanda ili kuziepusha kuvuka.

  1. Uzito wa Vitu

Ni muhimu kuchagua nguo zinazofaa kwa msimu husika. Kwa majira ya joto, unaweza kuchagua vitambaa vyepesi kama pamba, na kwa majira ya baridi, vitambaa vizito.

  1. Kujiamini

 Mavazi ya oversize yanataka mtu mwenye ujasiri, kwa sababu ni mtindo wa kipekee. Unapovaa nguo za oversize, hakikisha unajivunia kuvaa na unajiweka katika mwonekano wa kujiamini.

Hakikisha unapochagua mavazi ya oversize, unachagua sehemu moja tu kubwa na sehemu nyingine zikiwa za kawaida  ili kupunguza kupoteza muonekano wa kawaida.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags