Maajabu ya S2kizzy na Diamond  kwenye ‘Holiday’ 

Maajabu ya S2kizzy na Diamond  kwenye ‘Holiday’ 

Ni wakati wa mapumziko (Holiday) watu wanatoka kwenda kujivinjari pamoja na familia zao.

Kama kawaida mapumziko yanahusisha burudani, kipindi hiki cha Holiday msanii Diamond platnumz aliwabariki mashabiki wake wimbo uitwao 'Holiday' ambao aliuachia Desemba 13, 2024 ukiwa na mashairi yanayohusu kipindi hiki cha mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Wimbo wa Holiday umerekodiwa chini ya studio za Pluto ambazo zinamilikiwa na Zombie 'S2kizzy', mmoja kati ya watayarishaji wa muziki bora kwa sasa Afrika Mashariki, ambaye tayari ametengeneza rekodi nyingi na kubwa Tanzania.

S2kizzy amefanikisha kutengeneza ngoma kubwa kama Komasava ambayo ni bonge la ngoma kwa mwaka 2024, Enjoy ya kwake Jux ft Diamond 2023, lakini pia alifanikiwa kuingia kuwania tuzo za Grammy kupitia albamu ya 'Don Juan' ya kwake 'Maluma' ambapo ameshiriki kutayarisha wimbo wa 'Mama Tetema' na nyingine nyingi.

Kwa mujibu wa Zombie wimbo wa Holiday ambao unasumbua kwa sasa ni moja kati ya nyimbo ambazo zimerekodiwa ndani ya muda mfupi na msanii Diamond Platnumz.

"Diamond alini-surprise sana wote tulijua ataimba Bongo Fleva mule ambayo imechanganyikana na Baibuda kwa sababu biti linaruhusu sana miondoko ya Baibuda," alisema S2kizzy. 

Holiday ambao umefanywa na watayarishaji wawili S2kizzy na Sushi B kutokea South Afrika.

 Zombi anasema kwa mara ya kwanza alipenda namna ambavyo Sushi anatayarisha ngoma zake, hivyo alimuomba amuelekeze baadhi ya vitu ndio ukawa mwanzo wa kutengeneza mdundo wa Holiday.

"Nilimcheki kabla nikamwambia napenda namna unavyofanya sound zako alafu nikamwambia hii sound tukichanganya na Bongo Fleva tutatoa kitu poa sana kwa hiyo  baadaye tukafanya ngoma na Diamond alafu nikamtumia Sushi aliipenda sana," alisema S2kizzy alipofanya mahojiano na Rick Media.

Wimbo huo ambao kwa sasa audio yake imesikilizwa zaidi ya mara laki sita kwenye mtandao wa YouTube huku tangu utoke ukitumiwa na zaidi ya watu 300 kila siku kwenye mtandao wa Instagram unafanya ngoma hiyo kuwindwa na wasanii wengi wakubwa kwa ajili ya kufanyiwa remix.

Holiday unaingia kwenye orodha ya nyimbo kubwa ambazo zilifanywa kwa ajili ya matukio au kipindi fulani na zikapokelewa vizuri kwa mashabiki.

Kama ilivyokuwa kwa wimbo Dayoo  'Huu Mwaka' ambao ulitoka Januari 1, 2024 na kufanya vizuri mpaka kufikia kusikilizwa kwa zaidi ya mara milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Lakini pia wimbo huo ulifanyiwa remix na Rayvanny ambapo lyrics video imefanikiwa kutazamwa kwa zaidi ya mara milioni 12 kwenye mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags