Ifahamu tamaduni ya kuomboleza kwa kukata vidole

Ifahamu tamaduni ya kuomboleza kwa kukata vidole

Kuishi kwingi kuona mengi, ndivyo walivyosema wahenga. Msemo huo unaendana na mila na desturi za nchini Papua New Guinea, ambapo moja ya desturi zinazoshangaza ni ile ya kabila la Huli ambalo wanawake hukata vidole vyao kama ishara ya majonzi wanapofiwa.

Katika jamii hiyo desturi ya kukata vidole ni sehemu ya maombolezo, ambayo huonyeshwa na wanawake kama ishara ya huzuni na maumivu wanayoyahisi baada ya kifo cha mpendwa wao.

Hata hivyo ni wanawake pekee ndiyo hukata kidole kwani inaaminika kuwa wao ndio wanabeba maumivu makubwa zaidi mtu anapofariki.Kwa kawaida, vidole vinakatwa kwa kutumia kisu au kitu chenye ncha kali, na mara nyingi huwa ni vidole vya mguu au mkono.

Hata hivyo, desturi hii imekuwa ikikosolewa na watu wengi miaka ya hivi karibuni, hususan kutokana na athari za kiafya inayoweza kutokea kutokana na kukatwa vidole.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags