Kipaji Cha Liydia Kilivyowakosha Mastaa

Kipaji Cha Liydia Kilivyowakosha Mastaa

Ukiwa ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii basi fika utakuwa umeshakutana na video ya binti huyu anayefahamika kwa jina la Lydia Marley ambaye aliwavutia wadau na mastaa wengi kufuatia uwezo wake mkubwa wa kuimba.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa binti huyo mastaa mbalimbali wamejitokeza katika upande wa komenti wakionesha kuvutiwa na kipaji hicho huku orodha ya mastaa hao ikiongozwa na Mbosso akiandika “Fundi”, naye “Aloooh” Kusah, Wolper “Wow”, Mwana FA “Noma’ na mwengineo.

Mbali na kupokea komenti nyingi za pongezi kutoka kwa mastaa hao lakini pia msanii Mbosso kupitia Instagram yake alishare video ya binti huyo huku akiomba mawasiliano yake ili aweze kufanya naye kazi.

“Naomba msaada wa kupata mawasiliano ya huyu dada, nataka kufanya naye kazi, Trust me anakitu kikubwa sana ndani yake,” ameandika Mbosso

Lydia Marley amewahi kushiriki kwenye jukwaa la kusaka vipaji vya kuimba nchini BSS msimu wa 14 na kufanikiwa kupenya mpaka Top 6.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags