Baada ya mwanamuziki kutoka Marekani, Kanye West kurepotiwa kurudisha utajiri wake na kumfanya kuwa msanii anayeongoza kwa utajiri duniani, hayimaye Ye amewatarifu mashabiki zake kuwa amerudi kwa kishindo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameshare taarifa iliyokuwa ikieleza kuwa amefikia utajiri wa dola bilioni 2.77 huku akiandika maneno yasemayo “La, la, la la” ambayo aliwahi kuyatamka kwenye moja ya nyimbo zake.
Wimbo huo uliyopo kwenye album ya Kanye ‘Graduation (2007)’, ulikuwa ukizungumzia kuhusiana na maswala mazima ya mafanikio, changamoto za kimaisha na uhuru wa kujieleza ukiwa na moja ya kipande kisemacho “Subiri hadi nipate pesa zangu sawa”.
Kwa mujibu wa ‘Erin Venture Service, msanii huyo amefanikiwa kuongeza mpunga wa kutosha Januari hii na kupelekea utajiri wake kupanda ambapo mpaka sasa anakadiriwa kufikia dola bilioni 2.77 . ongezeko la fedha hizo likitokana na muziki wake pamoja na bidhaa za chapa ya YEEZY.
Mwaka 2022 Kanye alikumbana na pigo kubwa la kifedha kufuatia na kauli zake kuhusiana na Wayahudi, tukio hilo lilipelekea kutengwa na makampuni makubwa kama Def Jam, JP Morgan Chase, na Balenciaga huku akipoteza ushirikiano wake na kampuni ya Adidas.
Leave a Reply