Jinsi ya kukabiliana na Msongo wa mawazo

Jinsi Ya Kukabiliana Na Msongo Wa Mawazo

Na Aisha Lungato 

Msongo wa Mawazo/Stress ni tatizo ambalo limeendelea kuwa tatizo sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo,Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili. 

Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi,lakini jambo la baraka ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika,hivyo
Ungana nami ili kujua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.

Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili.

Kuzingatia hilo kuna mambo kadha wa kadha yanayomkabili kila mwanadamu
1.  Kutojiamini
2. Kuogopa mabadiliko
3.  Kukosa mpango wa maisha
4. Kupuuza mahitaji muhimu ya binadamu ya:-  Mwil,  Roho, Akili
5.  Kuishi kwa kukata tama•Kuumwa kichwa, Kukosa nguvu za mwili (me+ke),  Matatizo makubwa ya familia, Kukosa upendo,Hasira za mara kwa mara, Waathirika wa msongo na kusambaratika 


Kila lika inakubwa na tatizo hili la Msongo wa Mawazo lakini nitajaribu kufafanua watu tofauti ambao hukubwa sana na tatizo hili 

Wazazi – sababu kubwa ni uchumi wa familia: Watoto wanaouwezo wa kukuhoji kwa nini wewe ni masikini, kushindwa kupeleka watoto shule, kushidwa kutatua matatizo hata madogo madogo ya Familia hapo lazima upate Msongo wa Mawazo.


Waajiri/Waajiriwa – Watu hawa hupatwa na tatizo hili na huwapelekea kuhamisha mambo ya kazini
wanapeleka nyumbani na ya nyumbani wanayapeleka kazini. Mfano mtu amegombana na wafanyakazi wenzake kwa makosa yake mwenyewe akarudi nyumbani na kuendelea na hali ile na kusababisha matatizo nyumbani kwake. 

Vijana na wanafunzi – Vijana wengi hukubwa na tatizo hili hasa katika maswala ya kiuchumi na kwa wanafunzi wengi kuingia katika Mapenzi wakiwa bado wapo shule huwasababishia msongo wa mawazo kwani tayari anakua kajipa majukum mengine. Mfano jana amegombana na mpenzi wake leo akienda shule hawezi kusoma vizuri atakua mtu mwenye mawazo kutokana na kilichomkuta siku iliyopita. 

Wanandoa – Wanandoa wengi  wana msongo na kukosa faraja. Wanaamini nje kuna faraja zaidi (nyumba ndogo)
Wakristo wanaweza kusoma vitabu hivi ili kupata maelezo (luka 24),  (matendo 11:28-30),  (yohana 18:14-27)

Mizigo inayochosha
~Watu wengi hupata Msongo wa mawazo kutokana na wao kutaka

~ kujitwika mizingo wasiyo weza kuibeba nitataja baadhi Kushindana na jirani
~ Kufanya mambo nje ya uwezo wako
Kupata bp, tumbo, kichwa, bila sababu
~Kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao huwezi kuwalea 


Msongo wa mawazo hujitambulisha sana kwa mwili, akili na roho

Akili – ikisikia juu ya jambo gumu inashindwa kulipokea.  Inapeleka kwa tumbo, tumbo linashindwa linaamua kutoa unaharisha ndipo mtu hupata vidonda vya tumbo na tumbo kupata maumivu makali.

JINSI YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO

      Jifunze Kukubali Changamoto, Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine.

Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.

      Jifunze kusema "hapana" hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.

 Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, Kunawakati huwa tunakua na kampani ya watu ambao kabisa unajua hawa wananisababishia msongo wa mawazo Mfano:- Upo katika mahusiano na mtu ambaye wewe unampenda lakini haonyeshi kujali upendo wako utajitahidi kupiga simu kutuma sms umweke karibu lakini yeye hajali, si busara ukaendelea kuumiza kichwa kwajili yake ni bora uachane nae mapema sana.

Pia hata marafi wapo maadhi ya marafiki wanaweza wakakusababishia msongo wa mawazo kutokana na wanayokufanyia kwa mfano rafiki anayekupenda wakati wa raha tu na anakukimbia ukiwa na shida huyo si mwema kwako atakufanya uwe na Msongo wa mawazo. Tembelea watu wanaokufanya ufurahi na jifunze kucheka na kufurahi. Epuka kakaa na watu ambao kwako ni kikwazo.

Itaendelea……………………………….

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post