Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Rapa Jay-Z amfungulie mashtaka Tony Buzbee, wakili wa mwanamke aliyedai kubakwa na rapa huyo mwaka 2000 kwenye hafla za tuzo za Muziki za MTV. Jay-Z ameendelea kuonyesha alivyochukizwa na tukio hilo ambapo ameripotiwa kumfungulia kesi mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina bandia 'Jane Doe'.
Jay-Z ambaye jina halisi ni Shawn Carter alitoa sababu tatu kwanini anawashitaki wakili Tony Buzbee na mteja wake Jane Doe, akisema kuwa mashtaka hayo ni mabaya kwa upande wake, matumizi mabaya ya mchakato na uendeshaji wa kesi hiyo pamoja na kashfa mbaya alizopewa dhidi ya Jane Doe.
Kesi ya Jane Doe dhidi ya rapa Jay-Z na Diddy ilifutiliwa mbali Februari 14, 2025 baada ya mawakili wa mwanamke huyo kusema amaeachilia madai hayo. Hata hivyo, Doe alikiri kuwa na tofauti katika kutoa taarifa za kesi hiyo kutokana na kumbukumbu zake lakini lisisitiza kuwa amebakwa.
Mwanasheria wa Jay Z alipongeza uamuzi wa kufuta kesi hiyo uliyochukuliwa na Jane Doe dhidi ya mteja wake.
"Kesi ya uongo dhidi ya Jay Z ambayo haikupaswa hata kufikishwa mahakamani, Imefutwa kabisa" alisema wakili Jay Z, Alex Spiro.
Utakumbuka, Kesi ya awali ambayo iliwasilishwa na Doe, Oktoba 20, 2024, ilidai kuwa Sean "Diddy" Combs alimnyanyasa kingono msichana huyo kwenye sherehe baada ya Tuzo za Muziki za MTV mwaka 2000 akiwa na miaka 13.
Katika malalamiko yaliyorekebishwa, yaliyowasilishwa Desemba 2024, 'Jay Z' aliongezwa kama mshtakiwa na akashutumiwa kwa ubakaji. Hata Hivyo Jay Z, alikanusha vikali madai hayo, huku akimtaka mlalamikaji 'Doe' kufungua kesi ya jinai na siyo ya madai kama alivyofanya endapo anaamini madai yake yana ukweli wowote dhidi yake.
Mapema mwaka huu mawakili wa mwanamke huyo walitoa taarifa ya mteja wao kufuta kesi dhidi ya Jay-Z na Diddy huku uamuzi huo ukiwa na kipengele cha kutofunguliwa tena kesi hiyo katika siku za mbele kwakuwa madai hayo hayakuwa na ukweli wowote uliyo thibitishwa.
Jay-Z amefikia maamuzi ya kumshtaki mwanamke huyo ikiwa ni wiki moja tu kupita tangu aripotiwe Kumshtaki wakili wake Tony Buzbee.

Leave a Reply