Diddy aongeza mawakili apate dhamana

Diddy aongeza mawakili apate dhamana

Nguli wa Hip Hop, Sean ‘Diddy’ Combs anapambana kujinasua kutoka kwenye mikono ya sheria baada ya kukusanya wanasheria mashuhuri kuhakikisha wanamtetea na kupata dhamana ya kutoka mahabusu zikiwa zimepita wiki mbili tangu alipotiwa nguvuni.

Ripoti zinafichua Diddy ameandaa jopo la wanasheria mahiri kuhakikisha wanamtetea kwa kuwasilisha hoja zenye nguvu kisheria ili kumtoa mahabusu kwa dhamana, hilo likiwa ni jaribio la tatu baada ya kugomewa dhamana mara mbili.

Chanzo kinafichua rapa huyo mwimbaji wa wimbo wa I Need a Girl, kilifichua Diddy ameongeza mawakili wawili kwenye timu yake ya wanasheria, Anthony Ricco na Alexandra Shapiro ili kuifanya timu hiyo kuwa na nguvu katika kutimiza lengo la kumtetea kwenye kesi ya jinai inayomkabili.

Imeelezwa Ricco ni moja ya wanasheria mahiri kabisa huko Marekani na Alexandra ndiye mwanasheria msomi anayetamba kwa sasa. Mambo yalivyo ni kwamba Diddy ni kama anaunda timu yake kabambe kabisa ya wanasheria ili kuhakikisha anashinda yanayomkabili.

Diddy alikamatwa huko Midtown Manhattan kwenye hoteli ya Park Hyatt New York, Septemba 16 na kufikishwa mahakamani siku iliyofuatia, alipofunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia.

Kukamatwa kwa Diddy kumekuja miezi sita tangu polisi walipovamia kwenye makazi yake huko Los Angeles na Miami katika uchunguzi wao wa masuala ya uhalifu wa kingono.

Baba huyo wa watoto saba amekana kutenda kosa lolote kutoka kwenye mashtaka yanayomkabili.

Rapa huyo alijitangaza kuwa hana hatia kwa mashtaka hayo na mwanasheria wake, Marc Agnifilo, alisema mtayarishaji huyo wa muzuki hana hatia na hakuna cha kuficha. Diddy aligomewa dhamana licha ya wanasheria wake mahiri kabisa kuweka bondi ya Dola 50 milioni na kuomba zuio la wageni wa kike kwenye nyumbani kwake huko Miami kwa kipindi chote cha kesi yake.

Hata hivyo, baada ya malumbano makubwa ya kisheria kati ya wanasheria upande wa mashtaka na watetezi na ndiyo jaji wa Andrew Carter alipokataa kumpa dhamana Diddy kwa sababu za kiusalama za mshtakiwa huyo.

Akiwa katika gereza hilo, awali Diddy aligoma kula kwa hofu ya kuwekewa sumu na hasa kwa sababu amekutana na watu aliwahi kuwa na rekodi nao mbaya alipokuwa uraiani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags