Cardi B: Acheni Kumsema Tyla

Cardi B: Acheni Kumsema Tyla

Rapa maarufu kutoka Marekani, Cardi B, ameonyesha kuguswa na maneno ya mashabiki kwa mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Tyla katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na mashabiki wake kwenye jukwaa la X Spaces, Cardi B alisema chuki za mitandaoni zinaweza kumvunja msanii moyo na kumnyima kujiamini kwa muda mrefu.

Cardi B, ambaye pia ni mama wa watoto watatu, aliwaleza watu namna alivyokumbana na maneno makali kuhusu mwonekano wake alipokuwa mjamzito.

“Watu wamekuwa wakimtolea maneno makali sana Tyla kwenye mtandao, na jambo la kushangaza ni kwamba yeye mwenyewe hata hajibu wala kuzungumzia chochote kuhusu hayo maneno.

“Kuna baadhi ya watu hawataki tu kuona msanii akifanikiwa au kuwa na furaha. Wanakushambulia hadi wanakuondolea nguvu za kufanya kazi, wanakuondolea hali yako ya kujiamini, na wanakuporomosha hadi unapoteza kabisa hamasa na furaha ya kufanya kile unachokipenda, achene kumsema huyu binti jamani”amesema Cardi

Aidha aliongezea kwa kueleza “kila nikifungua TikTok nakuta mashambulizi dhidi ya binti huyu lakini sijui haya maneno yametokea wapi,”
Utakumbuka kwa muda sasa mwanamuziki Tyla amekuwa akipokea maoni mbalimbali kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki wakimnanga kuhusiana na namna anavyouwacha wazi mwili wali wake (kuvaa uchi).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags