Blinky Bill:Ladha ya muziki wa Tanzania imepotea

Blinky Bill:Ladha ya muziki wa Tanzania imepotea

S.Mwanamuziki wa Kenya Blinky Bill amesema ladha ya muziki wa Tanzania imepotea. Amegusia 'Nikusaidiaje' ya Professor Jay ft Ferooz na 'Inaniuma sana' (Juma nature)

Msanii wa muziki wa Jazz, Blinky Bill kutoka Kenya, ameiambia Mwananchi Digital kuwa Tanzania imepoteza ladha ya muziki iliyokuwa ikifanya zamani.

Msanii huyo ambaye ametumbuiza leo ikiwa ni siku ya pili ya Tamasha la Sauti za Busara, lililoanza jana Februari 14,2025, amesema ladha ya nyimbo kama 'Nikusaidiaje' (Professor Jay ft Ferooz) 'Inaniuma sana' (Juma nature) kwa sasa haipo tena.

"Hawa wasanii wa sasa wanafanya pop sana. Lakini nahisi kuna kitu nilikuwa nakipata kwenye muziki wa Tanzania kwa sasa sijui nakipata wapi. Nadhani Amapiano imechukua nafasi sana, kuna kitu nakikosa,"amesema

Ameongezea kuwa kwa wasanii wa kiume nchini inatamani kufanya kazi na Professor Jay huku akikazia Zuchu anajua kuimba lakini chaguo lake kwenye kazi ni Nandy.

Mbali na madhaifu hayo anayoyaona kwenye muziki wa Bongo Fleva, amesema upande wa video wasanii wa Tanzania wamekuwa wakifanya uwekezaji wa kutosha.

"Napenda ubora wa video, naona uwekezaji ni mkubwa pesa inawekwa sana. Ukiona mtu kama Diamond, Harmonize unajua pesa imetumika. Lakini kwa Kenya tunahitaji uwekezaji ili twende mbele,"amemalizia na kuongeza muziki wa singeli uangaliwe kwa jicho pevu kwani unaupekee unaoweza kuitambulisha Tanzania zaidi.

Akimalizia kwa kuzungumzia jukwaa la Sauti za Busara 2025, amesema mwaka huu kuna utofauti mkubwa kutoka kwa mashabiki.

"Vibe jukwaani ni 'connection' hata kama mashabiki hawaujui wimbo. Nimekiona leo nilikuwa nikipiga wimbo naona mashabiki wanaonesha nguvu hicho kitu ni muhimu kwangu,"amemalizia






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags