Mwanamitindo na mwigizaji kutoka Marekani Paris Jackson ambaye pia ni mtoto wa marehemu Michael Jackson ametangaza kuvishwa pete na mchumba wake wa muda mrefu Justin Long.
Mapema jana Desemba 6, 2024 Paris alishare picha akiwa anavishwa pete na mpenzi wake huyo huku akiambatanisha na ujumbe wa kumtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa.
“Happy birthday, my sweet blue. Kuishi maisha na wewe kwa miaka hii iliyopita kumekuwa safari isiyoelezeka, na siwezi hata kuota mtu mwingine kamili zaidi wa kushirikiana naye. Asante kwa kuniruhusu kuwa wako. Nakupenda.” Ameandika Paris Jackson
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali wawili hao walianza mahusiano mwaka 2021.
Paris na kaka yake mkubwa Prince ni watoto wa Michael Jackson aliyozaa na msaidizi wake wa matibabu Debbie Rowe, wawili hao walifunga ndoa mwaka 1996 na kutalikiana mwaka 1999. Alipoulizwa kuhusu uvumi kwamba si mtoto wa kibiolojia wa Mfalme wa Pop, Paris alisisitiza kuwa Michael atakuwa baba yake daima.
Leave a Reply