Billnass na Rayvanny waiombea Kenya

Billnass na Rayvanny waiombea Kenya

Wanamuziki wa Bongo Fleva Nchini Rayvanny na Billnass wametuma salamu za pole na kuwaombea wananchi wa Kenya ambao wamejeruhiwa na wengine kuuwawa katika maandamano ya kupinga Muswada mpya wa fedha wa 2024.

Kupitia Instastory ya Rayvanny ame-share ujumbe wa kuwatia moyo wananchi wa Kenya kwa kueleza kuwa mungu yupo pamoja nao. “Mungu yuko nanyi ndugu zangu wa Kenya”

Kwa upande wa Bilnass yeye alionesha kuumizwa na matukio yanayotokea nchini kwa kubadirisha profile picha yake katika mtandao wake wa Instagram na kuweka bendera ya Kenya ikiwa ni kuonesha mshikamano na watu wa Kenya katika kipindi hiki.

Mastaaa wengine ambao wametoa pole na kuungana na Wakenya ni ‘Zari The Boss Lady’, kutoka Uganda, Simi kutoka Nigeria na mwanamuziki wa Tanzania Vanessa Mdee ambaye kwa sasa anaishi Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags