Billnass na Nandy watambulisha mjengo wao mpya

Billnass na Nandy watambulisha mjengo wao mpya

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Nandy amefichua mjengo wao mpya wa kwanza yeye na mumewe Billnass.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha video inayoonesha mjengo huo ikiambatana na ujumbe unaoeleza kuwa ni zawadi kwa ajili ya binti yao aitwaye Naya.

“Tulianza zamani bugana tena tukapendana na yeye, tulianza zamani utoto ujana kugombana kupatana na yeye tunamshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha ku-share na nyie hii furaha kubwa ya hatua ya maisha yetu! nyumba yetu ya kwanza katika ndoa na zawadi ya binti yetu mrembo Naya.

Ndoa ni baraka na baraka tumeziona. bila kusahau wote mliotu-support na mnaoendelea kutu-support hakika support yenu ni chachu kubwa sana kwenye kila hatua maishani mwetu. tunawapenda na hatutakuja waangusha” ameandika Nandy

Wawili hao walifunga ndoa Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach, Dar es Salaam na kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Naya Agosti 2022.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags