Billnass amkaribisha Marioo kwenye chama

Billnass amkaribisha Marioo kwenye chama

Baada ya jinsia ya mtoto wa Marioo na Paula kutambulika mwanamuziki wa Bongo Fleva  Billnass amemkaribisha marioo kwenye chama cha wazazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Billnass ali-share picha ya Marioo akiwa na familia ya mpenzi wake iliyoambatana na ujumbe wa kumkaribisha msanii huyo kwenye chama cha wazazi huku akiwaombea kwa Mungu awapatie binti mwema.

Wawili hao waliweka wazi kutarajia mtoto siku tano zilizopita katika kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa kuchapisha video ikiambatana na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa wanatarajia kuongeza mwanafamilia mpya hivi karibuni.

Kumbuka Billnas ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Naya ambaye amempata kwa mkewe Nandy.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags