Billnass achukua muongozo wa maadili BASATA

Billnass achukua muongozo wa maadili BASATA

Baada ya kufungiwa miezi mitatu kwa kutojihusisha na kazi za sanaa na ‘faini’ ya milioni tatu  mwanamuziki #Billnass naye amefika Baraza la Sanaa Taifa #BASATA na kupatiwa muongoza wa maadili katika kazi za #Sanaa.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa #BASATA wame-share picha ya Nenga akikabidhiwa muongozo huo  siku ya jana na Katibu Mtendaji #BASATA, Dkt Kedmon Mapana.

Billnass alifungiwa kutojihusisha na kazi za Sanaa Novemba 7 kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘#Ameyatimba’ wa #Whozu , ambao  maudhui ya video yake yanatajwa kukiuka kanuni za maadili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags